Luqman 31:31
لقمانأَلَمْ تَرَ أَنَّ ٱلْفُلْكَ تَجْرِى فِى ٱلْبَحْرِ بِنِعْمَتِ ٱللَّهِ لِيُرِيَكُم مِّنْ ءَايَـٰتِهِۦٓ ۚ إِنَّ فِى ذَٰلِكَ لَـَٔايَـٰتٍ لِّكُلِّ صَبَّارٍ شَكُورٍ
Kwani huoni kwamba merikebu hupita baharini kwa neema za Mwenyezi Mungu, ili kuwaonyesha baadhi ya Ishara zake? Hakika katika haya zipo Ishara kwa kila mwenye kusubiri na mwenye kushukuru.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Kwani huoni kwamba marikebu hupita baharini zikichukua neema za Mwenyezi Mungu, ili kukuonyesheni baadhi ya Ishara zake? Hakika katika haya zipo Ishara kwa kila mwenye kusubiri, mwenye kushukuru. [31]
[31] Ewe mtu! Huzitazami marikebu, vyombo vinavyo kwenda baharini kwa rehema ya Mwenyezi Mungu, vikichukua ndani yake bidhaa za kukupeni manufaa, ili Mwenyezi Mungu akuonyesheni baadhi ya maajabu ya uundaji wake, na dalili za uweza wake? Hakika katika hayo zimo Ishara kwa kila mwenye kuvumilia mitihani yake, mwenye kuzishukuru kwa neema zake.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Kwani huoni, ewe mtazamaji, kwamba majahazi yanayotembea baharini kwa amri ya Allah Mtukufu ni neema itokayo Kwake kwa viumbe Wake, Apate kuwaonyesha utendakazi Wake na hoja Zake kwenu za kuwafanya nyinyi mzingatie? Hakika katika kupitisha majahazi baharini kuna dalili nyingi kwa kila mvumilivu sana, wa kuyaepuka yaliyoharamishwa na Allah Mtukufu, na katika kumtii Yeye na kuyavumilia mambo yaliyokadiriwa na Yeye, mwingi wa kushukuru neema Zake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net