Luqman 31:30
لقمانذَٰلِكَ بِأَنَّ ٱللَّهَ هُوَ ٱلْحَقُّ وَأَنَّ مَا يَدْعُونَ مِن دُونِهِ ٱلْبَـٰطِلُ وَأَنَّ ٱللَّهَ هُوَ ٱلْعَلِىُّ ٱلْكَبِيرُ
Hivi ni kwa sababu, Mwenyezi Mungu ndiye wa kweli, na hakika wanachokiomba ni cha uongo. Na kwamba hakika Mwenyezi Mungu ndiye Mtukufu na ndiye Mkubwa.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hivi ni kwa sababu hakika Mwenyezi Mungu ndiye wa kweli, na hakika wanacho kiomba ni cha uwongo. Na kwamba hakika Mwenyezi Mungu ndiye Mtukufu na ndiye Mkubwa. [30]
[30] Hayo yaliyo tajwa ni katika ajabu za uundaji wa Mwenyezi Mungu na uweza wake, kwa sababu muundaji wake ni Mungu aliye thibiti Ungu wake, Mwenye kustahiki peke yake kuabudiwa, na kwamba miungu yote mnayo iabudu badala yake ni miungu ya uwongo. Na hakika Mwenyezi Mungu, peke yake, ndiye Mtukufu wa shani, Mkubwa wa utawala.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Yote hayo ni miongoni mwa ukubwa wa uwezo Wake. Mpate kujua na mkubali kuwa Allah Mtukufu Ndiye wa kweli katika dhati Yake na sifa Zake na matendo Yake, na kuwa vile wanavyoviomba visivyokuwa Yeye ndio vya urongo, na kuwa Allah Mtukufu Ndiye Aliyetukuka, kwa dhati Yake, uwezo Wake na kutendesha nguvu Kwake, Aliye juu ya viumbe Vyake vyote, Aliye Mkubwa juu ya kila kitu, na kila kisichokuwa Yeye kinanyenyekea Kwake, Yeye Peke Yake Ndiye Anayestahiki kuabudiwa, na si mwingine.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net