Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 31 · Aya ya 17

Luqman 31:17

لقمان

يَـٰبُنَىَّ أَقِمِ ٱلصَّلَوٰةَ وَأْمُرْ بِٱلْمَعْرُوفِ وَٱنْهَ عَنِ ٱلْمُنكَرِ وَٱصْبِرْ عَلَىٰ مَآ أَصَابَكَ ۖ إِنَّ ذَٰلِكَ مِنْ عَزْمِ ٱلْأُمُورِ

Maana

Ewe mwanangu, shika Swala, na amrisha mema, na kataza maovu, na subiri kwa yanayokupata. Hayo ni katika mambo ya kuazimiwa.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Ewe mwanangu! Shika Swala, na amrisha mema, na kataza maovu, na subiri kwa yanayo kupata. Hayo ni katika mambo ya kuazimiwa. [17]

[17] Ewe mwanangu! Zihifadhi Swala, na amrisha kila wema, na kataza kila baya, na stahamili kwa shida zinazo kusibu. Hakika anayo usia Mwenyezi Mungu ni katika mambo ambayo yanahitajia kufanyiwa hima na kuyashikilia.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Ewe mwanangu! Simamisha Swala kikamilifu kwa kutimiza nguzo zake, sharti zake na mambo ya lazima yake, na uamrishe mema na ukataze maovu, na ujue kwamba nyasia hizi ni miongoni mwa mambo Aliyoyaamrisha Allah Mtukufu ambayo inatakiwa kuyafanyia pupa.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Luqman

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net