Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 31 · Aya ya 16

Luqman 31:16

لقمان

يَـٰبُنَىَّ إِنَّهَآ إِن تَكُ مِثْقَالَ حَبَّةٍ مِّنْ خَرْدَلٍ فَتَكُن فِى صَخْرَةٍ أَوْ فِى ٱلسَّمَـٰوَٰتِ أَوْ فِى ٱلْأَرْضِ يَأْتِ بِهَا ٱللَّهُ ۚ إِنَّ ٱللَّهَ لَطِيفٌ خَبِيرٌ

Maana

"Ewe mwanangu, kikiwapo kitu cha uzito wa chembe ya khardali kikawa ndani ya jabali au ndani ya mbingu au ndani ya ardhi, basi Mwenyezi Mungu atakileta. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa yaliyofichika, Mwenye habari za yote.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Ewe mwanangu! Kikiwapo kitu cha uzito wa chembe ya khardali kikawa ndani ya jabali au ndani ya mbingu au ndani ya ardhi, basi Mwenyezi Mungu atakileta. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa yaliyo fichika, Mwenye khabari za yote. [16]

[16] Ewe mwanangu! Hakika wema au ubaya kwa mtu, hata ukiwa, mathalan, kwa udogo wake kama chembe ya khardali, iliyoko pahali palipo fichikana kabisa, kama ndani ya jabali, au ndani ya mbingu, au chini ya ardhi, Mwenyezi Mungu ataufichua na autolee hisabu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mjuzi wa yaliyo fichika, hakifichikani kitu hata kidogo kwake, ni Mwenye khabari ya kujua hakika ya kila kitu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Ewe mwanangu! Jua kwamba uovu au wema uwapo ni kadiri ya chembe ya hardali, nayo ni ile yenye upeo wa udogo zaidi, iliyo ndani ya jabali au iliyo mahali popote, mbinguni au ardhini, Allah Mtukufu Ataileta Siku ya Kiyama na Ataihesabu. Hakika Allah Mtukufu ni Mpole kwa waja Wake, ni Mtambuzi wa matendo yao.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Luqman

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net