Ar-Room 30:32
الروممِنَ ٱلَّذِينَ فَرَّقُوا۟ دِينَهُمْ وَكَانُوا۟ شِيَعًا ۖ كُلُّ حِزْبٍۭ بِمَا لَدَيْهِمْ فَرِحُونَ
Katika wale ambao kwamba wameigawanya dini yao, na wakawa makundi makundi, kila kikundi kinafurahia kilicho nacho.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Katika wale ambao kwamba wameigawanya dini yao, na wakawa makundi makundi, kila kikundi kinafurahia kilicho nacho.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na msiwe ni miongoni mwa washirikina na watu wa (kufuata) matamanio na mambo ya uzushi, walioibadilisha dini yao na wakaigeuza kwa kuchukuwa baadhi yake na kuacha baadhi yake kwa kufuata matamanio yao, wakawa ni makundi na mapote, wanafuata maelekezo ya viongozi wao na vyama vyao na maoni yao, wanasaidiana wao kwa wao katika batili, kila watu wa kundi wanashangilia na kufurahia kundi lao, wanajihukumia wenyewe kuwa wao wako kwenye haki na wasiokuwa wao wako kwenye ubatilifu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net