Ar-Room 30:31
الروممُنِيبِينَ إِلَيْهِ وَٱتَّقُوهُ وَأَقِيمُوا۟ ٱلصَّلَوٰةَ وَلَا تَكُونُوا۟ مِنَ ٱلْمُشْرِكِينَ
Muwe wenye kutubia kwake, na mcheni Yeye, na simamisheni Swala, na wala msiwe katika washirikina.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Muwe wenye kutubia kwake, na mcheni Yeye, na shikeni Swala, na wala msiwe katika washirikina.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na muwe ni wenye kurejea kwa Allah Mtukufu kwa kutubia na kumtakasia matendo mema. Na muogopeni Yeye kwa kufanya maamrisho na kujiepusha na makatazo, na msimamishe Swala kikamilifu kwa nguzo zake na mambo yake yanayopasa na sharti zake, na msiwe ni miongoni mwa wenye kumshirikisha mwingine pamoja na Allah Mtukufu katika ibada.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net