Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 3 · Aya ya 8

Aal-i-Imraan 3:8

آل عمران

رَبَّنَا لَا تُزِغْ قُلُوبَنَا بَعْدَ إِذْ هَدَيْتَنَا وَهَبْ لَنَا مِن لَّدُنكَ رَحْمَةً ۚ إِنَّكَ أَنتَ ٱلْوَهَّابُ

Maana

(Na wao husema) Mola wetu Mlezi! Usizipotoe nyoyo zetu baada ya kutuongoa, na tutunuku rehema itokayo kwako. Hakika, Wewe ndiye Mwenye kutunuku mno.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

(Na hao husema): Mola wetu Mlezi! Usizipotoe nyoyo zetu baada ya kwisha tuongoa, na utupe rehema itokayo kwako. Hakika Wewe ndiye Mpaji. [8]

[8] Hao wanazuoni wenye akili husema: Mola wetu Mlezi! Usizifanye nyoyo zetu zikaacha Haki baada ya Wewe kwisha tuongoza kuiendea hiyo Haki. Ewe Mola wetu Mlezi! Tupe rehema kutoka kwako kwa kutuwezesha na kututhibitisha. Hakika Wewe ndiwe Mwenye kunyima na ndiwe Mpaji.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na wanasema, Ewe Mola wetu, usizipotoe nyoyo zetu na kukuamini Wewe, baada ya kutuneemesha kwa uongofu wa kufuata Dini Yako; na utupe miongoni mwa fadhila zako, rehema yenye kuenea. Kwani Wewe Ndiye Mpaji: Mwingi wa fadhila na kutoa, unampa unayemtaka bila ya hesabu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Aal-i-Imraan

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net