Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 3 · Aya ya 45

Aal-i-Imraan 3:45

آل عمران

إِذْ قَالَتِ ٱلْمَلَـٰٓئِكَةُ يَـٰمَرْيَمُ إِنَّ ٱللَّهَ يُبَشِّرُكِ بِكَلِمَةٍ مِّنْهُ ٱسْمُهُ ٱلْمَسِيحُ عِيسَى ٱبْنُ مَرْيَمَ وَجِيهًا فِى ٱلدُّنْيَا وَٱلْـَٔاخِرَةِ وَمِنَ ٱلْمُقَرَّبِينَ

Maana

Pale Malaika waliposema: Ewe Maryam! Hakika, Mwenyezi Mungu anakupa bishara njema ya (mwana kwa) neno litokalo kwake. Jina lake ni Masihi Isa mwana wa Maryam, mwenye heshima katika dunia na Akhera, na ni miongoni mwa waliowekwa karibu (na Mwenyezi Mungu).

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na pale Malaika walipo sema: Ewe Maryamu! Hakika Mwenyezi Mungu anakubashiria (mwana) kwa neno litokalo kwake. Jina lake ni Masihi Isa mwana wa Maryamu, mwenye hishima katika dunia na Akhera, na miongoni mwa walio karibishwa (kwa Mwenyezi Mungu). [45]

[45] Kumbuka na utaje ewe Nabii, pale Malaika walipo mbashiria Maryamu kuwa atamzaa mwana kwa neno lake tu Mwenyezi Mungu kinyume na ada wanavyo zaliwa watu. Jina lake mwana huyo ni Masihi Isa bin Maryamu. Na Mwenyezi Mungu amemjaalia hapa duniani kuwa atakuwa na cheo kwa unabii wake na kuepukana na aibu zote, na kesho Akhera kuwa atakuwa na cheo cha juu pamoja na kundi la walio takasika, wakawa wenye kuwa karibu mno na Mwenyezi Mungu miongoni mwa Manabii walio imara baraabara.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Kadhalika hukuwako huko, ewe Nabii wa Allah Mtukufu, pindi Malaika waliposema, Ewe Maryam, Allah Mtukufu Anakubashiria mtoto ambaye kupatikana kwake kutatokana na neno la Allah Mtukufu, yaani Atamwambia, ‘Kuwa,’ na atakuwa, jina lake ni Al-Masîḥ ‛Ĩsã mwana wa Maryam. Yeye atakuwa na jaha katika ulimwengu na Akhera na atakuwa ni miongoni mwa wenye kukurubishwa kwa Allah Mtukufu Siku ya Kiyama.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Aal-i-Imraan

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net