Aal-i-Imraan 3:44
آل عمرانذَٰلِكَ مِنْ أَنۢبَآءِ ٱلْغَيْبِ نُوحِيهِ إِلَيْكَ ۚ وَمَا كُنتَ لَدَيْهِمْ إِذْ يُلْقُونَ أَقْلَـٰمَهُمْ أَيُّهُمْ يَكْفُلُ مَرْيَمَ وَمَا كُنتَ لَدَيْهِمْ إِذْ يَخْتَصِمُونَ
Hizi ni katika habari za ghaibu tunazokufunulia. Nawe hukuwa nao walipokuwa wakitupa kalamu zao ni nani wao atakayemlea Maryam? Na hukuwa nao walipokuwa wakizozana.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hizi ni khabari za ghaibu tunazo kufunulia; nawe hukuwa nao walipo kuwa wakitupa kalamu zao nani wao atamlea Maryamu, na hukuwa nao walipo kuwa wakishindana. [44]
[44] Haya unayo simuliwa wewe Muhammad na Qur'ani ni katika khabari tukufu za wale alio wateuwa Mwenyezi Mungu, nazo ni khabari za ghaibu ambazo Mwenyezi Mungu anakufunulia. Na wala wewe hukuwapo wakati walipo kuwa wakipiga kura kwa mishale, ili waweze kukata shauri juu ya Maryamu. Na wala wewe hukuwapo walipo gombana kuwania nani wa kupata cheo hicho kitukufu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hizo tulizokusimulia, ewe Mtume, ni miongoni mwa habari za ghaibu alizokujulisha Allah Mtukufu kwa njia ya wahyi. Kwani wewe hukuwa pamoja na wao walipotafautiana juu ya nani mwenye haki zaidi na anayefaa kumlea Maryam, ukatokea utesi baina yao, wakapiga kura kwa kuzitupa kalamu zao, ikamwangukia Zakariyyã akapata ushindi wa kumlea.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net