Al-Ankaboot 29:8
العنكبوتوَوَصَّيْنَا ٱلْإِنسَـٰنَ بِوَٰلِدَيْهِ حُسْنًا ۖ وَإِن جَـٰهَدَاكَ لِتُشْرِكَ بِى مَا لَيْسَ لَكَ بِهِۦ عِلْمٌ فَلَا تُطِعْهُمَآ ۚ إِلَىَّ مَرْجِعُكُمْ فَأُنَبِّئُكُم بِمَا كُنتُمْ تَعْمَلُونَ
Na tumemuusia mwanadamu kuwafanyia wema wazazi wake. Na ikiwa watapambana nawe ili unishirikishe Mimi na yale usiyokuwa na elimu nayo, basi usiwatii. Kwangu Mimi ndiyo marejeo yenu, na nitawaambia yale mliyokuwa mkiyatenda.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na tumemuusia mwanaadamu kuwafanyia wema wazazi wake. Na ikiwa watakushikilia unishirikishe Mimi na usiyo kuwa na ujuzi nayo, basi usiwat'ii. Kwangu Mimi ndio marejeo yenu, na nitakwambieni mliyo kuwa mkiyatenda.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na tumemsihi binadamu awatendee wema wazazi wake wawili na awe mwema kwao wa maneno na vitendo. Na wakikushawishi ewe binadamu, umshirikishe mwingine na mimi katika ibada yangu, basi usifuate amri yao. Matakwa ya kuwa Allah Mtukufu ashirikishwe yanashikanishwa na matakwa ya kuwa vitendo vingine vya maasia vifanywe. Kwani hakuna kutiiwa kiumbe namna atakavyokuwa katika jambo la kumuasi Allah Mtukufu, Aliyetukuka, kama lilivyothibiti hilo kutoka kwa Mtume wa Allah Mtukufu, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie). Kwangu mimi ndio mwisho wenu, Siku ya Kiyama, na huko niwape habari ya matendo mema na mabaya ambayo mlikuwa mkiyafanya duniani na niwalipe kwa hayo.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net