Al-Ankaboot 29:69
العنكبوتوَٱلَّذِينَ جَـٰهَدُوا۟ فِينَا لَنَهْدِيَنَّهُمْ سُبُلَنَا ۚ وَإِنَّ ٱللَّهَ لَمَعَ ٱلْمُحْسِنِينَ
Na wale wanaofanya juhudi kwa ajili yetu, Sisi hakika tutawaongoa kwenye njia zetu. Na hakika Mwenyezi Mungu yu pamoja na watu wema.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na wanao fanya juhudi kwa ajili yetu, Sisi tutawaongoa kwenye njia zetu. Na hakika Mwenyezi Mungu yu pamoja na watu wema.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na Waumini waliopigana jihadi na maadui wa Allah Mtukufu, nafsi na Shetani na wakavumilia kwenye misukosuko na kero katika njia ya Allah Mtukufu, basi Allah Mtukufu Atawaongoa kwenye wema na kuwasimamisha imara juu ya njia iliyolingana sawa. Na yoyote ambaye sifa yake ni hii, basi yeye amejifanyia wema nafsi yake na amewafanyia wema wengine. Na Allah Mtukufu, Aliyetakasika na kuwa juu, Yupo pamoja na wale viumbe wake waliofanya wema, kwa kuwapa ushindi, kuwatilia nguvu, kuwahifadhi na kuwaongoza.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net