Al-Ankaboot 29:68
العنكبوتوَمَنْ أَظْلَمُ مِمَّنِ ٱفْتَرَىٰ عَلَى ٱللَّهِ كَذِبًا أَوْ كَذَّبَ بِٱلْحَقِّ لَمَّا جَآءَهُۥٓ ۚ أَلَيْسَ فِى جَهَنَّمَ مَثْوًى لِّلْكَـٰفِرِينَ
Na ni nani dhalimu mkubwa kuliko yule anayemzulia uongo Mwenyezi Mungu au anayekadhibisha Haki inapomjia? Je, si katika Jahannamu ndiyo yatakuwa makazi ya makafiri?
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na nani dhaalimu mkubwa kuliko yule anaye mzulia uwongo Mwenyezi Mungu au anaye kanusha Haki inapo mjia? Je! Si katika Jahannamu ndio yatakuwa makaazi ya makafiri?
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hakuna yoyote aliye na udhalimu mkubwa kuliko yule aliyemkanusha Allah Mtukufu na akamnasibishia Allah Mtukufu upotevu na ubatilifu, au akaikanusha haki ambayo Allah Mtukufu Amemleta nayo Mtume Wake Muhammad, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie). Hakika ndani ya Moto ni makao ya aliyemkanusha Allah Mtukufu na akaukataa upweke Wake na akamkanusha Mtume Wake Muhammad, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie).
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net