Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 28 · Aya ya 4

Al-Qasas 28:4

القصص

إِنَّ فِرْعَوْنَ عَلَا فِى ٱلْأَرْضِ وَجَعَلَ أَهْلَهَا شِيَعًا يَسْتَضْعِفُ طَآئِفَةً مِّنْهُمْ يُذَبِّحُ أَبْنَآءَهُمْ وَيَسْتَحْىِۦ نِسَآءَهُمْ ۚ إِنَّهُۥ كَانَ مِنَ ٱلْمُفْسِدِينَ

Maana

Hakika Firauni alitakabari katika ardhi, na akawagawa wananchi makundi mbali mbali. Akalidhoofisha taifa moja miongoni mwao, akiwachinja watoto wao wanaume na akiwaacha hai watoto wao wanawake. Hakika yeye alikuwa katika waharibifu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Hakika Firauni alitakabari katika nchi, na akawagawa wananchi makundi mbali mbali. Akalidhoofisha taifa moja miongoni mwao, akiwachinja watoto wao wanaume na akiwaacha watoto wao wanawake. Hakika yeye alikuwa katika mafisadi. [4]

[4] Hakika Firauni alipandwa na kiburi, na akapita mipaka katika udhalimu wake, na akatakabari mno katika nchi ya Misri. Akawafanya watu wa nchi hiyo makundi makundi, akiwanyanyua baadhi yao na akiwadhalilisha wenginewe, na khasa aliwadhoofisha Wana wa Israili. Akawa anawachinja watoto wao wanaume na akiwabakisha wanawake. Kwa hakika huyo alikuwa ni katika walio pita hadi katika ujabari na ufisadi.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hakika Firáwn alifanya kiburi na akapita mipaka katika nchi, akawafanya watu wake kuwa ni makundi tafauti tafauti, akawa analinyongesha kundi moja ya hayo, nalo ni lile la Wana wa Isrãîl, akawa anawaua watoto wao wa kiume na anawabakisha wanawake wao kwa kutumika na kudharauliwa, Hakika yeye alikuwa ni miongoni mwa waharibifu katika ardhi.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Qasas

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net