Al-Qasas 28:3
القصصنَتْلُوا۟ عَلَيْكَ مِن نَّبَإِ مُوسَىٰ وَفِرْعَوْنَ بِٱلْحَقِّ لِقَوْمٍ يُؤْمِنُونَ
Tunakusomea katika habari za Musa na Firauni kwa Haki kwa ajili ya watu wanaoamini.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Tunakusomea khabari za Musa na Firauni kwa Haki kwa ajili ya watu wanao amini. [3]
[3] Tunakusimulia baadhi ya khabari za Musa na Firauni kwa ukweli, ili wapate kuzizingatia Waumini.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Tunakusimulia wewe habari ya Mûsã na Firáwn kwa ukweli (ili wazingatie wale) watu wanaoiamini hii Qur’ani na wakubali kwamba inatoka kwa Allah Mtukufu na wafanye matendo yanayoambatana na uongofu wake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net