Al-Qasas 28:25
القصصفَجَآءَتْهُ إِحْدَىٰهُمَا تَمْشِى عَلَى ٱسْتِحْيَآءٍ قَالَتْ إِنَّ أَبِى يَدْعُوكَ لِيَجْزِيَكَ أَجْرَ مَا سَقَيْتَ لَنَا ۚ فَلَمَّا جَآءَهُۥ وَقَصَّ عَلَيْهِ ٱلْقَصَصَ قَالَ لَا تَخَفْ ۖ نَجَوْتَ مِنَ ٱلْقَوْمِ ٱلظَّـٰلِمِينَ
Basi mmoja katika wale wanawake wawili akamjia, naye anaona haya. Akasema, "Hakika baba yangu anakuita akulipe ujira wa kutunyweshea." Basi alipomjia na akamsimulia visa vyake, alisema, "Usihofu; umekwishaokoka kutokana na watu hao madhalimu."
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Basi mmoja katika wale wanawake wawili akamjia, naye anaona haya. Akasema: Baba yangu anakwita akulipe ujira wa kutunyweshea. Basi alipo mjia na akamsimulia visa vyake, alisema: Usiogope; umekwisha okoka kwenye watu madhaalimu. [25]
[25] Mmmoja wa wale mabinti akaja na ujumbe kutoka kwa baba yake baada ya kwisha jua khabari za Musa na wao wale mabinti. Naye akaja na huku anaona haya. Akasema: Baba yangu anakwita ili akulipe ujira kwa ulivyo tunyweshea maji. Basi alipo kwenda kwake na akamsimulia kisa chake cha kutoka Misri, akasema yule mzazi wa mabinti: Usikhofu; umekwisha okoka kwa hao watu madhaalimu. Kwani Firauni hana madaraka juu yetu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hapo akaja mmoja wa wale wanawake wawili aliyewachotea maji akitembea na huku yuwaona haya akasema, «Baba yangu anakuita ili akupe malipo ya maji uliyotuchotea.» Na Mûsã akaenda naye hadi kwa baba yake. Alipomjia baba yake na akamsimulia habari zake yeye pamoja na Firáwn na watu wake, yule baba wa mwanamke alisema, «Usiogope! Umeokoka na watu madhalimu, nao ni Firáwn na watu wake, kwani wao hawana mamlaka yoyote nchini kwetu».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net