Al-Qasas 28:24
القصصفَسَقَىٰ لَهُمَا ثُمَّ تَوَلَّىٰٓ إِلَى ٱلظِّلِّ فَقَالَ رَبِّ إِنِّى لِمَآ أَنزَلْتَ إِلَىَّ مِنْ خَيْرٍ فَقِيرٌ
Basi Musa akawanyweshea; kisha akarudi kivulini, na akasema, "Mola wangu Mlezi, hakika mimi ni mhitaji wa heri utakayoniteremshia."
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Basi Musa akawanyweshea; kisha akarudi kivulini, na akasema: Mola wangu Mlezi! Hakika mimi ni mhitaji wa kheri utakayo niteremshia. [24]
[24] Musa akajitolea kuwakhudumia akawanyweshea. Kisha akenda kuegemea mti akipumzika baada ya kuhangaika kule, naye akisema kwa unyenyekevu: Ewe Mola wangu Mlezi! Hakika mimi ni mwenye haja ya kheri yoyote na riziki yoyote utayo niletea.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Basi Mûsã akawachotea maji wanyama wa wale wanawake wawili, kisha akageuka kwenda kwenye kivuli cha mti kujifunika nacho na akasema, «Mola wangu! Hakika mimi ni mhitaji wa wema wako wowote ule utakaoniletea,» kama vile chakula. Na njaa ilikuwa imemshika sana.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net