Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 28 · Aya ya 16

Al-Qasas 28:16

القصص

قَالَ رَبِّ إِنِّى ظَلَمْتُ نَفْسِى فَٱغْفِرْ لِى فَغَفَرَ لَهُۥٓ ۚ إِنَّهُۥ هُوَ ٱلْغَفُورُ ٱلرَّحِيمُ

Maana

Akasema, "Mola wangu Mlezi, hakika mimi nimejidhulumu mwenyewe. Basi nisamehe." Kwa hivyo, akamsamehe; hakika Yeye ni Mwingi wa kusamehe, Mwingi wa kurehemu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Akasema: Mola wangu Mlezi! Hakika mimi nimejidhulumu nafsi yangu; basi nisamehe. Akamsamehe; hakika Yeye ni Mwenye kusamehe Mwenye kurehemu. [16]

[16] Musa akasema kwa kunyenyekea kwa Mwenyezi Mungu na majuto: Ewe Mola wangu Mlezi! Mimi nimejidhulumu nafsi yangu kwa niliyo yatenda. Basi nighufirie kitendo changu hichi. Mwenyezi Mungu akamuitikia ombi lake na akamsamehe. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mkuu wa kusamehe, Mkunjufu wa rehema.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Mûsã akasema, «Mola wangu! Mimi nimejidhulumu nafsi yangu kwa kumuua mtu ambaye hukuniamuru kumuua, basi nisamehe dhambi hiyo.» Na Allah Mtukufu Akamsamehe. Kwani Allah Mtukufu ni Mwenye kusamehe sana dhambi za waja Wake, ni Mwenye huruma nao sana.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Qasas

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net