Ash-Shu'araa 26:8
الشعراءإِنَّ فِى ذَٰلِكَ لَـَٔايَةً ۖ وَمَا كَانَ أَكْثَرُهُم مُّؤْمِنِينَ
Hakika katika haya zipo Ishara. Lakini wengi wao hawakuwa wenye kuamini.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hakika katika haya zipo Ishara. Lakini wengi wao hawakuwa wenye kuamini. [8]
[8] Hakika katika kutoka kwa hii mimea ni dalili kubwa ya kuwepo Muumba Muweza. Lakini wengi wa watu si wenye kuamini.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Kwa hakika, katika kuitoa mimea kwenye ardhi ni dalili ya wazi ya ukamilifu wa uwezo wa Allah Mtukufu, na wengi wa watu hawakuwa ni wenye kuamini.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net