Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 26 · Aya ya 7

Ash-Shu'araa 26:7

الشعراء

أَوَلَمْ يَرَوْا۟ إِلَى ٱلْأَرْضِ كَمْ أَنۢبَتْنَا فِيهَا مِن كُلِّ زَوْجٍ كَرِيمٍ

Maana

Je, hawakuiona ardhi, ni mimea mingapi tumeiotesha humo, ya kila namna nzuri?

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Je! Hawakuiona ardhi, mimea mingapi tumeiotesha humo, ya kila namna nzuri? [7]

[7] Hivyo hao wanatenda watendavyo katika ukafiri wao na kukadhibisha kwao wala hawaangalii baadhi ya uumbaji wa Mwenyezi Mungu katika hii hii ardhi? Lau kuwa wanaangalia kwa kuzingatia wangeli ongoka. Hebu wazingatie hii mimea ya kila namna yenye manufaa tunayo itoa Sisi kwenye ardhi, na wala hawezi hayo isipo kuwa Mungu Mmoja Muweza.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Je, wanakanusha na hali wao hawakuiangalia ardhi ambayo ndani yake tumeotesha kila aina nzuri ya mimea ambayo hakuna awezae kuiyotesha isipokuwa Mola wa viumbe vyote?

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Ash-Shu'araa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net