Ash-Shu'araa 26:53
الشعراءفَأَرْسَلَ فِرْعَوْنُ فِى ٱلْمَدَآئِنِ حَـٰشِرِينَ
Basi Firauni akawatuma mijini wakusanyaji.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Basi Firauni akawatuma mijini wapiga mbiu za mgambo. [53]
[53] Firauni akawatuma askari wake katika miji ya mamlaka yake, wawakusanye wenye maguvu katika kaumu yake, alipo jua kuwa Musa kesha toka na Wana wa Israili, ili awazuie lile walilo kusudia.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Fir’awn akawatuma askari wake, alipopata habari kwamba Wana wa Isrãîl wameenda usiku, wakusanye jeshi lake kutoka miji ya utawala wake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net