Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 26 · Aya ya 52

Ash-Shu'araa 26:52

الشعراء

وَأَوْحَيْنَآ إِلَىٰ مُوسَىٰٓ أَنْ أَسْرِ بِعِبَادِىٓ إِنَّكُم مُّتَّبَعُونَ

Maana

Na tulimuamrisha Musa kwa ufunuo: Nenda na waja wangu wakati wa usiku. Kwa hakika mtafuatwa.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na tulimuamrisha Musa kwa wahyi: Nenda na waja wangu wakati wa usiku. Kwa hakika mtafuatwa. [52]

[52] Na Mwenyezi Mungu alimpa wahyi Musa a.s. atoke usiku usiku pamoja na Waumini miongoni mwa Wana wa Israili, ilipo kuwa tena haiwi kumsubirisha Musa. Mpango ukawa wa makundi mawili kwamba atangulie Musa na kaumu yake, na Firauni afuatie na kaumu yake, mpaka waingie katika maingilio ya njia ya baharini, na Mwenyezi Mungu awateketeze.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na Allah Mtukufu Akampelekea wahyi Mûsã, amani imshukie, kwamba, «Nenda usiku pamoja na walioamini miongoni mwa Wana wa Isrãîl, ili Fir’awn na askari wake, ambao watawafuata nyinyi, wasije wakawafikia kabla ya kufika kwenu baharini».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Ash-Shu'araa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net