Ash-Shu'araa 26:204
الشعراءأَفَبِعَذَابِنَا يَسْتَعْجِلُونَ
Basi je, wanaihimiza adhabu yetu?
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Basi, je, wanaihimiza adhabu yetu?. [204]
[204] Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu: Watu wa Makka wameghurika na kuchelewesha kwangu kuwaadhibu, basi ndio wanaihimiza? Anakusudia Subhanahu Aliye takasika kuzisafihi akili zao kwa sababu ya kuhimiza kwao adhabu juu ya kuwaonya na kuwatisha.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Je, hawa wamedanganyika na kule kuwapa muhula kwangu ndipo wakawa wanataka kuteremka adhabu kwa haraka juu yao kutoka mbinguni?
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net