Ash-Shu'araa 26:203
الشعراءفَيَقُولُوا۟ هَلْ نَحْنُ مُنظَرُونَ
Na watasema: "Je, tutapewa muhula?"
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na watasema: Je, tutapewa muhula?. [203]
[203] Watasema itapo teremka hiyo adhabu: Je, tutapewa muhula? Haya ni kwa majuto kwa kupitiwa na Imani na kutaka waakhirishiwe adhabu. Lakini hawajibiwi.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na hapo waseme, watakaposhtushwa nayo, kwa majuto, «Je, sisi ni wenye kupatiwa nafasi na kucheleweshwa tupate kutubia kwa Allah Mtukufu ushirikina wetu na tuyafanye yaliyotupita?»
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net