Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 25 · Aya ya 9

Al-Furqaan 25:9

الفرقان

ٱنظُرْ كَيْفَ ضَرَبُوا۟ لَكَ ٱلْأَمْثَـٰلَ فَضَلُّوا۟ فَلَا يَسْتَطِيعُونَ سَبِيلًا

Maana

Tazama jinsi wanavyokupigia mifano. Basi wamepotea, wala hawataiweza Njia.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Tazama jinsi wanavyo kupigia mifano. Basi wamepotea, wala hawataiweza Njia. [9]

[9] Hebu angalia, ewe Nabii! Vipi wanavyo kupigia mifano hawa! Mara wanakupigia mfano wa mwenye kurogwa, mara nyengine kuwa ati ni mwendawazimu, mara ya tatu kuwa ni mwongo, na mara yane kuwa unaipokea Qur'ani kutokana na wasio kuwa Waarabu. Hao kwa hayo hakika wameipotea njia ya haki, na kuhojiana kulio sawa. Basi hawaitambui njia ya kufikilia yote hayo.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Tazama, ewe Mtume, namna walivyosema, hawa wakanushaji, juu yako maneno hayo ya ajabu yanayofanana na mifano kwa ugeni wake, ili wafikie kukukanusha, kwa hivyo wakawa mbali na haki, na kwa hivyo hawapati njia ya kuifikia (hiyo haki) ili wayarekebishe maneno waliyoyasema kuhusu wewe, ya urongo na uzushi.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Furqaan

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net