Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 25 · Aya ya 10

Al-Furqaan 25:10

الفرقان

تَبَارَكَ ٱلَّذِىٓ إِن شَآءَ جَعَلَ لَكَ خَيْرًا مِّن ذَٰلِكَ جَنَّـٰتٍ تَجْرِى مِن تَحْتِهَا ٱلْأَنْهَـٰرُ وَيَجْعَل لَّكَ قُصُورًۢا

Maana

Ametukuka ambaye akitaka atakujalia yaliyo bora kuliko hayo, nayo ni mabustani yapitayo mito kati yake, na atakujaalia majumba ya fahari.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Ametukuka ambaye akitaka atakujaalia yaliyo bora kuliko hayo,nayo ni mabustani yapitayo mito kati yao, na atakujaalia majumba ya fakhari. [10]

[10] Mwenyezi Mungu ametukuka, na izidi kheri yake! Yeye ndiye ambaye pindi akitaka atakujaalia duniani bora kuliko hayo wanayo pendekeza wao. Kwa Akhera Yeye amekwisha kujaalia kama alivyo kuahidi, nayo ni mabustani mengi yapitayo mito pembezoni mwake, na baina ya miti yake, na majumba ya fakhari madhubuti.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Ni kubwa mno baraka za Allah Mtukufu, na ni mengi sana mema Yake, Ambaye angetaka kukufanyia mema zaidi kuliko yale waliotamani uwe nayo, Angekufanyia ulimwenguni, mashamba mengi ambayo kati yake inapita mito, na Akufanye uwe na majumba makubwa ya fahari.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Furqaan

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net