An-Noor 24:48
النوروَإِذَا دُعُوٓا۟ إِلَى ٱللَّهِ وَرَسُولِهِۦ لِيَحْكُمَ بَيْنَهُمْ إِذَا فَرِيقٌ مِّنْهُم مُّعْرِضُونَ
Na wanapoitwa kumuendea Mwenyezi Mungu na Mtume wake ili ahukumu baina yao, kipo kikundi katika wao kinakataa.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na wanapo itwa kumuendea Mwenyezi Mungu na Mtume wake ili ahukumu baina yao, kipo kikundi katika wao kinakataa. [48]
[48] Na katika hali zao ni kuwa wakitakiwa kuhukumiwa mbele ya Mtume kwa jambo alilo literemsha Mwenyezi Mungu, unaafiki wa baadhi yao hudhihiri, na wao hukataa kuhukumiwa wakijua kuwa haki ni ya wale makhasimu zao.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na wanapoitwa, wanapokuwa kwenye ugomvi baina yao, kwenye hukumu iliyo ndani ya Kitabu cha Allah Mtukufu na waje kwa Mtume ili afanye uamuzi kati yao, ghafla hujitokeza kikundi kati yao kikajiepusha na kikawa hakikubali hukumu ya Allah Mtukufu na Mtume Wake, pamoja na kuwa hiyo ndiyo haki isiyo na shaka.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net