Al-Muminoon 23:99
المؤمنونحَتَّىٰٓ إِذَا جَآءَ أَحَدَهُمُ ٱلْمَوْتُ قَالَ رَبِّ ٱرْجِعُونِ
Mpaka yanapomfikia mmoja wao mauti, husema: "Mola wangu Mlezi! Nirudishe.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Mpaka yanapo mfikia mmoja wao mauti, husema: Mola wangu Mlezi! Nirudishe. [99]
[99] Wanaendelea kuwakanusha mpaka utapo fika wakati wa kufa mmoja wao hujuta na akasema: Ewe Mola wangu Mlezi! Nirudishe duniani.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Allah Mtukufu Anawatolea habari makafiri au waliokiuka mipaka ya amri Yake, na walioko kwenye hali ya kusongwa na kifo, kuwa mauti yanapowafikia na wakaishuhudia adhabu waliyoandaliwa, huwa anasema kila mmoja wao, Mola wangu! nirudishe ulimwenguni.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net