Al-Muminoon 23:96
المؤمنونٱدْفَعْ بِٱلَّتِى هِىَ أَحْسَنُ ٱلسَّيِّئَةَ ۚ نَحْنُ أَعْلَمُ بِمَا يَصِفُونَ
Kinga maovu kwa kutenda yaliyo mema zaidi. Sisi tunayajua vyema wayasemayo.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Kinga maovu kwa kutenda yaliyo mema zaidi. Sisi tunajua wayasemayo. [96]
[96] Wewe endelea na wito wako, na ukabili uovu wao kwa vitendo vilivyo vizuri kama kusamehe au vyenginevyo. Na Sisi tunajua vyema wanakutaja vipi wewe, na wanavyo usema kwa ubaya huo wito wako kwa uwovu na uzushi. Na Sisi tutawalipa kwa hayo.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Pindi wanapokufanyia ubaya maadui zako, ewe Mtume, kwa maneno au vitendo, basi usiwalipe ubaya, lakini uondoshe ubaya wao kwa kuwafanyia wema. Sisi tunayajua mno yale wanayokubandika washirikina ya sifa za ushirikina na kukukanusha, na tutawalipa kwa hayo malipo maovu mno.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net