Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 23 · Aya ya 89

Al-Muminoon 23:89

المؤمنون

سَيَقُولُونَ لِلَّهِ ۚ قُلْ فَأَنَّىٰ تُسْحَرُونَ

Maana

Watasema, "Ufalme huo ni wa Mwenyezi Mungu." Sema: Basi vipi mnadanganyika?

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Watasema: (Ufalme huo) ni wa Mwenyezi Mungu. Sema: Basi vipi mnadanganyika? [89]

[89] Watakiri kuwa hakika huyo ni Mwenyezi Mungu. Waambie: Basi huwaje mkadanganyika kwa pumbao na kuchochewa na mashetani, na mkaacha ut'iifu wa Mwenyezi Mungu?

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Watajibu kuwa hayo yote ni ya Allah Mtukufu. Sema uwaambie, «Vipi zinaondoka akili zenu na mnadanganywa na mnateneanishwa na njia ya kumpwekesha Allah Mtukufu na kumtii na kuyaamini mambo ya kufufuliwa na kurudishiwa uhai?»

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Muminoon

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net