Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 23 · Aya ya 88

Al-Muminoon 23:88

المؤمنون

قُلْ مَنۢ بِيَدِهِۦ مَلَكُوتُ كُلِّ شَىْءٍ وَهُوَ يُجِيرُ وَلَا يُجَارُ عَلَيْهِ إِن كُنتُمْ تَعْلَمُونَ

Maana

Sema: Ni nani mkononi mwake umo Ufalme wa kila kitu, naye ndiye anayelinda, wala hakilindwi asichotaka, kama mnajua?

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Sema: Ni nani mkononi mwake umo Ufalme wa kila kitu, naye ndiye anaye linda, wala hakilindwi asicho taka, kama mnajua? [88]

[88] Waambie vile vile: Nani mwenye ufalme wa kila kitu mkononi mwake, na mwenye madaraka yasio na ukomo katika kila kitu, na ambaye ndiye kwa uwezo wake analinda kila kitu, wala hayamkiniki yeyote kumlinda yeyote na adhabu yake? Kama nyinyi mnaijua jawabu, basi nijibuni.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Sema, «Ni nani mmiliki wa kila kitu? Na ni nani Ambaye mkononi Mwake kuna hazina za kila kitu? Na ni nani Anayempa himaya mwenye kutaka himaya Yake, ambapo hakuna anayeweza kumhami na kumlinda yule ambaye Allah Mtukufu Anataka kumuangamiza wala hakuna anayekinga shari Aliyoikadiria Allah Mtukufu, iwapo mnalijua hilo?»

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Muminoon

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net