Al-Muminoon 23:83
المؤمنونلَقَدْ وُعِدْنَا نَحْنُ وَءَابَآؤُنَا هَـٰذَا مِن قَبْلُ إِنْ هَـٰذَآ إِلَّآ أَسَـٰطِيرُ ٱلْأَوَّلِينَ
Tuliahidiwa haya sisi na baba zetu wa zamani. Hayakuwa haya ila ni visa vya uongo vya watu wa zamani.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Tuliahidiwa haya sisi na baba zetu zamani. Hayakuwa haya ila ni visa vya uwongo vya watu wa zamani. [83]
[83] Sisi tuliahidiwa haya, na pia baba zetu waliahidiwa hayo hayo hapo zamani. Haya si chochote ila ni ahadi za uwongo walizo buni watu wa zamani.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Yameshasemwa maneno haya kuambiwa wazee wetu kitambo, kama vile unavyotuambia, ewe Muhammad, hatukuyaona kuwa yana uhakika. Hayakuwa haya isipokuwa ni porojo za watu wa kale.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net