Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 23 · Aya ya 82

Al-Muminoon 23:82

المؤمنون

قَالُوٓا۟ أَءِذَا مِتْنَا وَكُنَّا تُرَابًا وَعِظَـٰمًا أَءِنَّا لَمَبْعُوثُونَ

Maana

Walisema: Je, tukishakufa tukawa udongo na mifupa, ndio tutafufuliwa?

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Walisema: Je! Tukisha kufa tukawa udongo na mifupa ndio tutafufuliwa? [82]

[82] Katika kukanusha kwao kufufuliwa, walisema: Hivyo sisi tutafufuliwa baada ya kwisha geuka mchanga na mifupa?

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Walisema «Ati tutakapokufa na miili yetu ikatangamana na mchanga wa ardhi pamoja na mifupa yetu tutafufuliwa mara nyingine? Hili haliwi wala haliingii akilini».

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Muminoon

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net