Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 23 · Aya ya 72

Al-Muminoon 23:72

المؤمنون

أَمْ تَسْـَٔلُهُمْ خَرْجًا فَخَرَاجُ رَبِّكَ خَيْرٌ ۖ وَهُوَ خَيْرُ ٱلرَّٰزِقِينَ

Maana

Au unawaomba ujira? Lakini ujira wa Mola wako Mlezi ni bora, na Yeye ndiye Mbora wa wanaoruzuku.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Au unawaomba ujira? Lakini ujira wa Mola wako Mlezi ni bora, na Yeye ndiye Mbora wa wanao ruzuku. [72]

[72] Kwani, ewe Nabii! Unawataka ujira kwa huku kufikisha kwako ujumbe? Hayakuwa hayo! Kwa kuwa ujira hakika ujira wa Mola wako Mlezi ni bora zaidi kuliko walio nao wao; na Yeye ndiye Mbora wa kutoa.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Au limewazuia wao kukuamini kwa kuwa wewe, ewe Mtume, unawaomba malipo juu ya ulinganizi wako kwao? hivyo basi wakafanya ubahili? Hukufanya hivyo, kwa kuwa zile thawabu zilizoko kwa Allah Mtukufu na vipewa ni bora zaidi. Na Yeye ni bora wa wanaoruzuku, hakuna awezaye kuruzuku kama Yeye Anavyoruzuku, kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake na kutukuka ni Kwake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Muminoon

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net