Al-Muminoon 23:63
المؤمنونبَلْ قُلُوبُهُمْ فِى غَمْرَةٍ مِّنْ هَـٰذَا وَلَهُمْ أَعْمَـٰلٌ مِّن دُونِ ذَٰلِكَ هُمْ لَهَا عَـٰمِلُونَ
Lakini nyoyo zao zimefunikwa hazitambui hayo, na wanavyo vitendo vinginevyo wanavyovifanya.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Lakini nyoyo zao zimeghafilika na hayo, na wanavyo vitendo vinginevyo wanavyo vifanya. [63]
[63] Lakini makafiri kwa sababu ya inadi yao na chuki zao ni wenye kughafilika na kufanya kheri, na kujikalifu kufanya liwezekanalo, na kwamba kuna hisabu ya kuchungua kila kitu. Na mbali na hayo bado wanavyo vitendo vingine viovu wanavyo dumu navyo.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Lakini nyoyo za makafiri ziko kwenye upotevu uliowafunika, zimejiepusha na Qur’ani na yaliyomo ndani yake. Na wao, pamoja na ushirikina wao, wana matendo mabaya, Allah Mtukufu anawapa muhula wayafanye, ili ziwapate wao hasira za Allah Mtukufu na mateso Yake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net