Al-Muminoon 23:62
المؤمنونوَلَا نُكَلِّفُ نَفْسًا إِلَّا وُسْعَهَا ۖ وَلَدَيْنَا كِتَـٰبٌ يَنطِقُ بِٱلْحَقِّ ۚ وَهُمْ لَا يُظْلَمُونَ
Na hatuitwiki nafsi isipokuwa kwa kiasi cha uwezo wake. Na tunacho kitabu kisemacho kweli. Nao hawatadhulumiwa.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na hatuilazimishi nafsi ila kwa kadri ya uwezo wake. Na tunacho kitabu kisemacho kweli. Nao hawatadhulumiwa. [62]
[62] Na Sisi hatumlazimishi mtu yeyote ila kwa analo liweza kulifanya, kwa sababu limo ndani ya makdara yake. Na kila a'mali katika a'mali za waja zimesajiliwa kwetu katika kitabu, na tutawapa khabari zake kama zilivyo. Na wao hawatadhulumiwa kwa kuongezewa adhabu wala kupunguziwa thawabu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hatumlazimishi mja yoyote miongoni mwa waja wetu isipokuwa kile kinachomkunjukia kukifanya, na matendo yao yamesajiliwa kwetu ndani ya Kitabu cha kudhibiti matendo, ambacho Malaika watakiinua, kitakachosema ukweli juu yao, na hakuna yoyote kati yao Atakayedhulumiwa.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net