Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 23 · Aya ya 53

Al-Muminoon 23:53

المؤمنون

فَتَقَطَّعُوٓا۟ أَمْرَهُم بَيْنَهُمْ زُبُرًا ۖ كُلُّ حِزْبٍۭ بِمَا لَدَيْهِمْ فَرِحُونَ

Maana

Lakini walikatiana jambo lao mapande mbalimbali. Kila kundi likifurahia kwa waliyo nayo.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Lakini walikatiana jambo lao mapande mbali mbali. Kila kundi likifurahia kwa waliyo nayo. [53]

[53] Lakini watu walilikata kata hili jambo la Dini yao. Wapo kati yao walio ongoka, na wapo walio potoka ambao wakafuata matamanio yao, wakafarikiana kwa sababu hiyo wakawa makundi mbali mbali yenye kufanyiana uadui. Kila kikundi kinafurahi kwa walio nayo, kwa kudhania kuwa wao tu ndio walio sibu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na wafuasi walifarikiana katika dini wakawa makundi na mapote, wakaifanya dini yao kuwa dini nyingi baada ya kuamrishwa wajikusanye pamoja. Kila kundi linajigamba kwa maoni yake, linadai kuwa kundi hilo liko kwenye haki na lingine liko kwenye batili. Katika haya pana onyo la kujiweka kwenye makundi na kufarikiana katika Dini.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Muminoon

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net