Al-Muminoon 23:52
المؤمنونوَإِنَّ هَـٰذِهِۦٓ أُمَّتُكُمْ أُمَّةً وَٰحِدَةً وَأَنَا۠ رَبُّكُمْ فَٱتَّقُونِ
Na kwa yakini huu Umma wenu ni Umma mmoja, na Mimi ni Mola wenu Mlezi, basi nicheni Mimi.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na kwa yakini huu Umma wenu ni Umma mmoja, na Mimi ni Mola wenu Mlezi, basi nicheni Mimi. [52]
[52] Na tukawaambia wawafikishie watu wao: Hakika hii Dini niliyo kutumeni muifikishe ni Dini moja kwa mintarafu ya Imani na misingi ya sharia. Na hakika nyinyi ni umma mmoja katika vizazi vyote. Miongoni mwao wapo walio ongoka, na wapo walio potoka. Na Mimi ndiye Mola wenu Mlezi niliye kuamrisheni muifuate, basi iogopeni adhabu yangu pindi mkiasi.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na kwa hakika Dini yenu, enyi Mitume, ni Dini moja, nayo ni Uislamu, na mimi ni Mola wenu niogopeni kwa kufuata maamrisho yangu na kujiepusha na makatazo yangu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net