Al-Muminoon 23:38
المؤمنونإِنْ هُوَ إِلَّا رَجُلٌ ٱفْتَرَىٰ عَلَى ٱللَّهِ كَذِبًا وَمَا نَحْنُ لَهُۥ بِمُؤْمِنِينَ
Huyu si lolote isipokuwa ni mwanamume anayemzulia Mwenyezi Mungu uongo, wala sisi sio wa kumuamini.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Huyu si lolote ila ni mtu anaye mzulia Mwenyezi Mungu uwongo, wala sisi sio wa kumuamini. [38]
[38] Huyu si chochote ila ni mtu aliye mzulia Mwenyezi Mungu, na akadai kwamba Mwenyezi Mungu kamtuma yeye. Na amesema uwongo katika hayo anayo tuitia. Wala hatutomsadiki abadan. *
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na huyu, Anayewalingania kwenye Imani, hakuwa isipokuwa ni mtu amemzulia Allah Mtukufu urongo. Na sisi si wenye kuyaamini anayoyasema.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net