Al-Muminoon 23:37
المؤمنونإِنْ هِىَ إِلَّا حَيَاتُنَا ٱلدُّنْيَا نَمُوتُ وَنَحْيَا وَمَا نَحْنُ بِمَبْعُوثِينَ
Hapana isipokuwa uhai wetu wa duniani tu, tunakufa na kuishi tu. Wala sisi hatutafufuliwa.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hapana ila uhai wetu wa duniani tu, tunakufa na kuishi basi. Wala sisi hatutafufuliwa. [37]
[37] Hapana uhai ila mmoja tu. Nao ndio huu uhai wa duniani, ambao tunauona una mauti na uhai unao tupitia. Kinacho zaliwa kinazaliwa, na kilicho hai kinakufa. Wala hatutofufuliwa baada ya kwisha kufa kabisa.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Maisha yetu ni ya hapa duniani tu, wazazi wanakufa na watoto wanaishi. Na sisi si wenye kutolewa tukiwa hai mara nyingine.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net