Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 23 · Aya ya 21

Al-Muminoon 23:21

المؤمنون

وَإِنَّ لَكُمْ فِى ٱلْأَنْعَـٰمِ لَعِبْرَةً ۖ نُّسْقِيكُم مِّمَّا فِى بُطُونِهَا وَلَكُمْ فِيهَا مَنَـٰفِعُ كَثِيرَةٌ وَمِنْهَا تَأْكُلُونَ

Maana

Na hakika mnayo mazingatio makubwa katika wanyama wa kufugwa waliwao. Tunawanywesha nyinyi katika vile vilivyo matumboni mwao, na nyinyi mnapata katika hao manufaa mengi, na pia mnawala.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na hakika mnayo mazingatio makubwa katika nyama hoa - tunakunywesheni katika vile viliomo matumboni mwao, na nyinyi mnapata katika hao manufaa mengi, na pia mnawala. [21]

[21] Na nyinyi mnapata kutokana na nyama hoa, nyama wa kufuga, nao ni ngamia, ng'ombe, kondoo na mbuzi, mambo yanayo onyesha uwezo wetu na fadhila zetu juu yenu kwa kukuneemesheni. Tunakunywesheni kutoka matumboni mwao maziwa safi, matamu, mepesi kwa wenye kuyanywa. Na mbali ya maziwa mnapata manufaa mengine kama nyama, na sufi, na manyoya. Na kutokana na hao nyinyi mnaishi na mnaruzukiwa.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na nyinyi, enyi watu, mna mazingatio katika ngamia, ng’ombe, mbuzi na kondoo ya kulizingatia namna ya kuumbwa kwao. Tunawanywesha maziwa yanayotoka matumboni mwao. Na mnayo nyinyi kutokana nao manufaa mengine mengi kama sufi na ngozi na mfano wa hivyo, na miongoni mwavyo mnakula.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Muminoon

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net