Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 23 · Aya ya 17

Al-Muminoon 23:17

المؤمنون

وَلَقَدْ خَلَقْنَا فَوْقَكُمْ سَبْعَ طَرَآئِقَ وَمَا كُنَّا عَنِ ٱلْخَلْقِ غَـٰفِلِينَ

Maana

Na kwa yakini tumeziumba juu yenu njia saba. Nasi hatukuwa wenye kughafilika na viumbe.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na kwa yakini tumeziumba juu yenu njia saba. Nasi hatukuwa wenye kughafilika na viumbe. [17]

[17] Na hakika Sisi tumeziumba mbingu saba zilizo nyanyuka juu yenu. Ndani yake vipo viumbe ambavyo hatukughafilika navyo. Tunavihifadhi na tunaviendesha. Na Sisi kabisa hatughafiliki na viumbe vyetu vyote. Bali tunavilinda visipotee na kuharibika, na tunavipangia mambo yao yote kwa hikima. "Na kwa yakini tumeziumba juu yenu njia saba. Nasi hatukuwa wenye kughafilika na viumbe." Hizo njia saba zilizo tajwa katika hiyo Aya maana yake ni mbingu saba, na kwamba hizo si mbingu moja, na Mwenyezi Mungu haghafiliki na mbingu hizo na viumbe viliomo ndani yake.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Kwa hakika tuliziumba juu yenu mbingu saba, moja juu ya nyingine, na hatukuwa tumeghafilika na viumbe, hatughafiliki na kiumbe wala hatumsahau.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Muminoon

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net