Al-Hajj 22:55
الحجوَلَا يَزَالُ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ فِى مِرْيَةٍ مِّنْهُ حَتَّىٰ تَأْتِيَهُمُ ٱلسَّاعَةُ بَغْتَةً أَوْ يَأْتِيَهُمْ عَذَابُ يَوْمٍ عَقِيمٍ
Na waliokufuru hawataacha kuwa katika wasiwasi kwa hilo mpaka Saa ya Kiyama iwafikie ghafla, au iwafikie adhabu ya Siku Tasa.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na walio kufuru hawatoacha kuwa katika wasiwasi kwa hilo mpaka Saa iwafikie ghafla, au iwafikie adhabu ya Siku Tasa. [55]
[55] Na walio kufuru hawatengenei. Bali wanaendelea kuitilia shaka Qur'ani mpaka wafikiwe na mauti, iwafikie adhabu ya Siku isiyo kuwa na kheri kwao wala rehema; nayo ni Siku ya Kiyama.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na hawataacha makafiri wenye kukanusha kuendelea kuwa kwenye shaka juu ya Qur’ani uliokuja nayo, mpaka Kiyama kiwajie ghafla na hali wao wako juu ya ukanushaji wao, au iwajie adhabu ya Siku isiyokuwa na wema ndani yake, nayo ni Siku ya Kiyama.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net