Al-Hajj 22:54
الحجوَلِيَعْلَمَ ٱلَّذِينَ أُوتُوا۟ ٱلْعِلْمَ أَنَّهُ ٱلْحَقُّ مِن رَّبِّكَ فَيُؤْمِنُوا۟ بِهِۦ فَتُخْبِتَ لَهُۥ قُلُوبُهُمْ ۗ وَإِنَّ ٱللَّهَ لَهَادِ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓا۟ إِلَىٰ صِرَٰطٍ مُّسْتَقِيمٍ
Na ili waliopewa elimu wajue kuwa hayo ni Haki itokayo kwa Mola wako Mlezi na waamini, na zipate kutua nyoyo zao. Na hakika Mwenyezi Mungu ndiye anayewaongoa wenye kuamini kwenye njia iliyonyooka.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na ili walio pewa ilimu wajue kuwa hayo ni Haki itokayo kwa Mola wako Mlezi na waamini, na zipate kutua nyoyo zao. Na hakika Mwenyezi Mungu ndiye anaye waongoa wenye kuamini kwenye Njia Iliyo Nyooka. [54]
[54] Na ili walio pewa ilimu ya sharia na Imani wazidi Imani na kujua kwamba wayasemayo Mitume na Manabii hakika ni kweli iliyo teremka kutokana na Mwenyezi Mungu. Na kwamba Mwenyezi Mungu hakika anawalinda Waumini kwa hima yake kutokana na matatizo yote yanayo wapitikia. Na huwaongoa kwenye maarifa ya Njia Iliyo Nyooka nao wakaifuata.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na ili wapate kujua wenye elimu ambao wanapambanua, kwa ujuzi wao, baina ya ukweli na urongo kwamba Qur’ani tukufu ndio haki iliyoteremka juu yako, ewe Mtume, kutoka kwa Allah Mtukufu, haina udanganyifu ndani yake na hakuna njia yoyote ya Shetani kuifikia, na kwa hiyo imani yao inaongezeka na nyoyo zao zinainyenyekea. Na hakika ya Allah Mtukufu ni Mwenye kuwaongoa wale walioiamini na wakamuamini Mtume Wake kwenye njia ya haki iliyo wazi, nayo ni Uislamu, na Atawaokoa kwayo na upotevu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net