Al-Hajj 22:46
الحجأَفَلَمْ يَسِيرُوا۟ فِى ٱلْأَرْضِ فَتَكُونَ لَهُمْ قُلُوبٌ يَعْقِلُونَ بِهَآ أَوْ ءَاذَانٌ يَسْمَعُونَ بِهَا ۖ فَإِنَّهَا لَا تَعْمَى ٱلْأَبْصَـٰرُ وَلَـٰكِن تَعْمَى ٱلْقُلُوبُ ٱلَّتِى فِى ٱلصُّدُورِ
Je, hawatembei katika ardhi ili wapate kuwa na nyoyo za kuzingatia, au masikio ya kusikilia? Kwani hakika si macho yanayopofuka. Lakini zinazopofuka ni nyoyo zilizomo vifuani.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Je! Hawatembei katika ardhi ili wapate kuwa na nyoyo zao za kuzingatia, au masikio ya kusikilia? Kwani hakika si macho yanayo pofuka, lakini zinazo pofuka ni nyoyo ziliomo vifuani. [46]
[46] Hivyo wao wanasema wayasemayo na wanahimiza waletewe adhabu, nao hawatembei ulimwenguni wakaona kwa macho yao walivyo teketea hao madhaalimu wakanushao? Huenda hapo nyoyo zao zikagutuka kutokana na ghafla iliyo wapamba, na wakatia akilini yanao wapasa wakafuata hayo ya wito wa Haki unao waitia. Na masikio yao yakisikia vifo vya hao makafiri huenda wao wakazingatia. Lakini wapi! Ya mbali hayo kuwa watu hawa waweze kuzingatia kwa wanayo yaona au kuyasikia maadamu nyoyo zao zimekuwa kama mawe. Kwani kipofu wa kweli siye yule aliye pofuka macho, lakini ni yule aliye pofuka moyo na hatambui kitu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Si watembee hao wakanushaji wa Makureshi kwenye ardhi wajionee athari za walioangamizwa, wafikirie kwa akili zao na wazingatie, na wasikie habari zao kusikia kwa mazingatio wapate kuwaidhika? Kwani upofu si upofu wa macho, hakika ya upofu wenye kuangamiza ni upofu wa busara wa kutoijua haki na kutozingatia.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net