Al-Hajj 22:45
الحجفَكَأَيِّن مِّن قَرْيَةٍ أَهْلَكْنَـٰهَا وَهِىَ ظَالِمَةٌ فَهِىَ خَاوِيَةٌ عَلَىٰ عُرُوشِهَا وَبِئْرٍ مُّعَطَّلَةٍ وَقَصْرٍ مَّشِيدٍ
Basi ni miji mingapi iliyokuwa ikidhulumu tuliiangamiza, ikawa imebaki magofu, na visima vilivyoachwa, na majumba yaliyokuwa madhubuti?
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Miji mingapi tuliiangamiza iliyo kuwa ikidhulumu, ikawa imebaki magofu, na visima vilivyo achwa, na majumba yaliyo kuwa madhubuti? [45]
[45] Basi tuliwatekeza watu wengi wa miji ambayo waliiamirisha, kwa sababu ya udhalimu wao na kukanusha kwao Mitume wao. Zikawa paa za nyumba zao zimeangukia kuta zake, hazina wakaazi. Kama kwamba jana hazikuwapo. Visima vingapi vilivyo bomoka na maji yake yakapotea, na majumba mangapi madhubuti yaliyo jengwa kwa mawe na saruji na chokaa, yamekuwa magofu hayana wakaazi!
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Ni miji mingi iliyojidhulumu kwa ukafiri wake, tuliwaangamiza watu wake, nyumba zao zikavunjwa zikawa ziko tupu hazina wakazi wake, visima vyake vikawa havichotwi maji na majumba yake ya fahari yaliyo marefu yaliyopambwa hayakuwakinga watu wake na adhabu kali.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net