Al-Hajj 22:39
الحجأُذِنَ لِلَّذِينَ يُقَـٰتَلُونَ بِأَنَّهُمْ ظُلِمُوا۟ ۚ وَإِنَّ ٱللَّهَ عَلَىٰ نَصْرِهِمْ لَقَدِيرٌ
Wameruhusiwa kupigana wale wanaopigwa vita kwa sababu wamedhulumiwa - na kwa yakini Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kuwasaidia.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Wameruhusiwa kupigana wale wanao pigwa vita kwa sababu wamedhulumiwa - na kwa yakini Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kuwasaidia . [39]
[39] Mwenyezi Mungu amewaruhusu Waumini wanao pigwa vita na washirikina wawarejezee uadui wao, kwa sababu ya dhulma iliyo wapata nao wakasubiri kwa muda mrefu. Na hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuweza kuwanusuru vipenzi vyake Waumini. " Wameruhusiwa kupigana wale wanao pigwa vita kwa sababu wamedhulumiwa - na kwa yakini Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kuwasaidia" Yaliyo tajwa na Qur'ani Tukufu kukhusu hukumu iliomo katika Aya 39 yamezitangulia kanuni zilizo kuja kuwekwa na madola baada yake, nayo ni kuwa mtu kujitetea nafsi yake ni sharia vyovyote vile itavyo kuwa matokeo yake. Na kwamba mwenye kuitetea nafsi yake, na mali yake, na nchi yake, hawi ni mkosa mbele ya Mwenyezi Mungu na mbele ya uadilifu, ijapo kuwa ameuwa mtu au ameteketeza roho nyingi. Aya hii imepasisha kuwa Waislamu wanayo ruhusa kujitetea pindi wakivamiwa. Na kwa hivyo tunafahamu kuwa vita vya Waislamu vilikuwa vita vya utetezi na kujilinda si vita vya kushambulia na kuvamia. Na kwamba Waislamu waliusimamisha Uislamu na wakaupa nguvu kwa hoja zilizo wazi, na dalili zilizo dhaahiri.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Waislamu, mwanzo wao, walikuwa wamekatazwa kupigana na makafiri, wameamrishwa kuvumilia maudhi yao. Maudhi ya washirikina yalipofikia upeo wake na Mtume akatoka Makkah hali ya kuhama kwenda Madina na Uislamu ukawa na nguvu, Allah Mtukufu Aliwaruhusu Waislamu kupigana kwa sababu hiyo ya maonevu yaliyowashukia na uadui. Na Allah Mtukufu ni Muweza wa kuwanusuru na kuwadhalilisha maadui wao.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net