Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 21 · Aya ya 89

Al-Anbiyaa 21:89

الأنبياء

وَزَكَرِيَّآ إِذْ نَادَىٰ رَبَّهُۥ رَبِّ لَا تَذَرْنِى فَرْدًا وَأَنتَ خَيْرُ ٱلْوَٰرِثِينَ

Maana

Na Zakariya alipomwita Mola wake Mlezi: Mola wangu Mlezi! Usiniache peke yangu, na Wewe ndiye Mbora wa wanaorithi.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na Zakariya alipo mwita Mola wake Mlezi: Mola wangu Mlezi! Usiniache peke yangu, na Wewe ndiye Mbora wa wanao rithi. [89]

[89] Na kitaje kisa cha Zakariya alipo mwita Mola wake Mlezi baada ya kwisha ona uweza wake Subhanahu kwa alivyo mtia katika nafsi yake matarajio ya rehema yake. Alisema: Ewe Mola wangu Mlezi! Usiniache mpweke bila ya kuwa na mrithi, na Wewe ndiye Mbora wa wanao rithi. Kwani Wewe ndiye utakaye baki baada ya kumalizika viumbe vyote.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na kumbuka, ewe Mtume, kisa cha mja wa Allah Mtukufu Zakariyyâ alipomuomba Mola wake Amtunukie watoto, wakati umri wake ulipokuwa mkubwa, kwa kusema, «Mola wangu! Usiniache mpweke ni siwe na mtoto! Basi nitunuku mrithi wa kusimamia mambo ya Dini kwa watu baada yangu mimi, na wewe Ndiye bora wa wenye kusalia na bora wa wenye kusimamia mambo yangu baada yangu kwa uzuri!»

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Anbiyaa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net