Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 21 · Aya ya 67

Al-Anbiyaa 21:67

الأنبياء

أُفٍّ لَّكُمْ وَلِمَا تَعْبُدُونَ مِن دُونِ ٱللَّهِ ۖ أَفَلَا تَعْقِلُونَ

Maana

Aibu yenu nyinyi na hivyo mnavyoviabudu badala ya Mwenyezi Mungu! Basi nyinyi hamtii akilini?

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Aibu yenu nyinyi na hivyo mnavyo viabudu badala ya Mwenyezi Mungu! Basi nyinyi hamtii akilini? [67]

[67] Aibu yenu! Nyinyi na miungu yenu mmelaanika! Mnaacha fikra zenu zipotee, na mnapuuza kuzingatia? Bila ya shaka haya masanamu hayafai kuabudiwa!

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Ubaya ni wenu na ni wa waungu wenu mnaowaabudu badala ya Allah Mtukufu, Aliyetukuka. Kwani hamtii akili mkajua uovu wa haya mliyonayo?

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Al-Anbiyaa

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net