Al-Anbiyaa 21:66
الأنبياءقَالَ أَفَتَعْبُدُونَ مِن دُونِ ٱللَّهِ مَا لَا يَنفَعُكُمْ شَيْـًٔا وَلَا يَضُرُّكُمْ
Akasema: Basi nyinyi mnawaabudu wasiokuwa Mwenyezi Mungu wasiowafaa kitu wala kuwadhuru?
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Akasema: Basi nyinyi mnawaabudu asiye kuwa Mwenyezi Mungu wasio kufaini kitu wala kukudhuruni? [66]
[66] Ibrahim akasema: Ikiwa hali yao haya masanamu ni hii, hayawezi kitu, na nyinyi ndio makhusiano yenu nao ni hivi, basi nyinyi mmekuwa mnaacha kumuabudu Mwenyezi Mungu, na badala yake mnaabudu vitu visivyo kupeni faida hata chembe mkiviabudu, wala havikudhuruni kwa lolote mkiviachilia mbali?
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Ibrãhîm akasema kwa njia ya kudharau jambo la kuabubudu masanamu, «Vipi mnaabudu masanamu wasionufaisha wanapoabudiwa wala kudhurisha wanapoachwa?»
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net