Al-Anbiyaa 21:51
الأنبياءوَلَقَدْ ءَاتَيْنَآ إِبْرَٰهِيمَ رُشْدَهُۥ مِن قَبْلُ وَكُنَّا بِهِۦ عَـٰلِمِينَ
Na hakika tulikwishampa Ibrahim uongofu wake zamani, na tulikuwa tunamjua.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na hakika tulikwisha mpa Ibrahim uwongofu wake zamani, na tulikuwa tunamjua. [51]
[51] Na hakika Sisi tulikwisha mpa Ibrahim uwongofu na fikra ya kutafuta Haki kwa usafi wa niya kabla ya Musa na Haaruni. Na Sisi ni Wenye kujua vyema hali yake na fadhila zake zilizo mfanya astahiki kuchukua Utume.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Kwa hakika, tulimpa Ibrãhîm uongofu wake ambao yeye aliwalingania watu waufuate kabla ya Mûsã na Hãrûn. Na sisi tulikuwa tunajua kwamba yeye anastahiki hilo.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net